• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • SOKA: Bilionea Mohamed MO Dewji atangaza kujiuzulu uenyekiti Simba

  (GMT+08:00) 2020-01-14 10:22:30

  Mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi wa Simba SC bilionea Mohamed MO Dewji jana alifikia maamuzi mazito ya kutangaza kujiuzulu nafasi yake ya uenyekiti na kubakia kama muwekezaji wa Simba, MO amefikia hatua hiyo kutokana na timu hiyo kutofanya vizuri katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika wakitolewa na UD Songo ya Msumbiji hatua ya awali, sare ya 2-2 dhidi ya Yanga inayoonekana kupitia kipindi kigumu kiuchumi na kupoteza fainali ya jana ya Kombe la Mapinduzi 1-0 dhidi ya Mtibwa Suger. Kwenye ukurasa wake wa Twitter MO Dewji ameandika hivi

  "Ni aibu Simba kutoshinda, baada ya kulipa mishahara inayokaribia Bilioni 4 kwa mwaka, najiuzulu kama mwenyekiti wa bodi na kubakia muwekezaji, Simba Nguvu Moja, nitatia nguvu kwenye kuendeleza miundombinu na soka la vijana"

  Hii inakuwa ni fainali ya nne kwa Simba SC kuwahi kupoteza katika michuano ya Mapinduzi Cup kati ya 7, wakati Mtibwa Sugar hii ikiwa ni fainali yao ya pili kutwaa Ubingwa kati ya sita, inadaiwa kuwa MO Dewji msimu huu hajaridhishwa na kiwango cha Simba SC kabisa ikizingatiwa amefanya usajili mkubwa zaidi.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako