• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • TENISI: Serena Williams ashinda taji la WTA Auckland Classic baada ya miaka mitatu

    (GMT+08:00) 2020-01-14 10:22:46

    Nguli wa mchezo wa tenisi kwa wanawake Serena Williams, amefanikiwa kuchukua taji la michuano ya wazi ya WTA Auckland Classic baada ya Januari 12, 2020 kushinda fainali kwa seti 6-3, 6-4 dhidi ya Mmarekani mwenziwe Jessica Pegula. Taji hilo ni la kwanza kwa Serena baada ya miaka mitatu kupita tangu aliposhinda michuano ya wazi ya Australia mwaka 2017. Pia ni la kwanza tangu alipopata mtoto wake Alexis Olympia, Septemba 1, 2017. Sasa akiwa na umri wa miaka 38, amefikisha mataji 73 yanayotambuliwa na shirikisho la tenisi kwa wanawake WTA. Pia amecheza na kushinda mataji ndani ya miongo minne ambapo kwa mara ya kwanza alishinda ubingwa mwaka 1999. Baada ya kushinda ubingwa huo, Serena ametoa kiasi cha $43,000 zaidi ya shilingi milioni 90 kwa wahanga wa janga la moto kule nchini Australia ambapo ndio alichukua ubingwa wake wa mwisho mwaka 2017.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako