• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • KASHFA: Kesi ya mkuu wa zamani IAAF Lamine Diack yapigwa kalenda hadi Juni

    (GMT+08:00) 2020-01-14 10:23:41

    Kesi ya mkuu wa zamani wa Shirikisho la Riadha la Kimataifa IAAF Lamine Diack, ambaye anashutumiwa kupokea mamilioni ya fedha ili kuficha majibu ya vipimo vya dawa za kusisimua misuli ya Russia na kutakatisha pesa jana ilipigwa kalenda na kupangwa kusikilizwa tena mwezi Juni. Jaji anayeongoza kesi ya Msenegali huyo mwenye miaka 86 amesema wanahitaji muda zaidi wa kuchunguza ushuhuda uliotolewa na mwanawe ambaye naye pia ni mtuhumiwa, Papa Massata Diack, mwezi Novemba huko Senegal. Papa Massata Diack amekataa kutoa ushirikiano kwa mamlaka ya Ufaransa na kubaki hukohuko Senegal. Licha ya Ufaransa kutoa kibali cha kimataifa cha kumkamata, mamalaka ya Senegal wamesema hawatamkabidhi. Hata hivyo Diack junior, alihojiwa huko Dakar mwezi November juu ya shutuma dhidi yake na baba yake ukiwa ni uchunguzi unaofanywa na Senegal pekee.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako