• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • RIADHA: Brigid Kosgei kutetea rekodi yake ya London Marathon

  (GMT+08:00) 2020-01-14 16:30:36

  Mshikiliaji wa rekodi yam bio za Marathon duniani kwa wanawake, Brigid Kosgei wa Kenya ataungana na Mkenya mwenzake Eliud Kipchoge kutetea rekodi zao za mbio za Marathon za London April 26 mwaka huu. Brigid, ambaye aliweka rekodi mpya ya dunia kwa kutumia saa 2:14:04 Chicago mwezi Oktoba mwaka jana na kuvunja rekodi iliyowekwa na Mwingereza Paula Radcliffe kwa zaidi ya dakika moja, atakumbana na changamoto kubwa kutoka kwa mkimbiaji huyo mwenyeji atakayeshiriki mashindano hayo. Wakimbiaji wengine wanawake kutoka Kenya ni mshindi wa mbio za London Marathon mwaka 2018 Vivian Cheruiyot, mshindi mara tatu wa Berlin Marathon Gladys Cherono, na Ruth Chepngetich anayeshikilia rekodi ya sasa ya dunia.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako