• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • SOKA: Gor Mahia yasaini mshambuliaji kinda

  (GMT+08:00) 2020-01-14 16:31:47

  Mabingwa wa Ligi Kuu Kenya (KPL) Gor Mahia wamemsaini mshambuliaji anayeongoza kwa magoli katika Ligi ya Taifa ya daraja la Kwanza (NSL) Clinton Okoth anayechezea timu ya Migori Youth. Okoth mwenye umri wa miaka 19, pia alikuwa akifuatiliwa na timu nyingine zinazocheza Ligi Kuu ikiwemo KCB, AFC Leopards na Kariobangi Sharks. Mahambuliaji huyo anatarajiwa kuziba pengo lililoachwa wazi na Francis Afriyie na Gisleim Yikpe walioihama timu hiyo mwezi huu. Mwenyekiti wa timu ya Migori Youth Abdi Aziz amesema hatua hiyo ni nzuri kwa kijana huyo ambaye amekuwa katika klabu hiyo tangu akiwa na umri wa miaka 13.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako