• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Biashara ya nje ya China yaongezeka kwa asilimia 3.4 kwa mwaka jana

  (GMT+08:00) 2020-01-14 16:46:08

  Thamani ya biashara ya nje ya China imeongezeka kwa asilimia 3.4 katika mwaka 2019 na kufikia dola za kimarekani trilioni 4.6.

  Takwimu zilizotolewa na Mamlaka Kuu ya Forodha ya China zimeonyesha kuwa, biashara ya nje ilikua kwa asilimia 5 ikilinganishwa na kipindi kama hicho mwaka 2018, huku uagizaji wa bidhaa nao ukiongezeka kwa asilimia 1.6.

  Makamu mkuu wa Mamlaka hiyo Zou Zhiwu amesema, China inatarajia kuendelea kuwa nchi kubwa kibiashara duniani kwa mwaka 2020. Amesema biashara ya nje ya China kwa mwaka jana ilikua kwa utulivu na kwa ubora zaidi licha ya changamoto za ndani na nje ya nchi.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako