• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Nchi za Afrika zachangia dola milioni 141 za kimarekani katika mfuko wa Amani wa dunia kuanzia mwaka 2017

  (GMT+08:00) 2020-01-14 18:48:45

  Kamati ya Umoja wa Afrika imesema kuwa, mchango wa kifedha wa nchi wanachama wa Umoja huo kwenye Mfuko wa Amani wa Umoja wa Afrika umepita dola za kimarekani milioni 141 katika kipindi cha miaka mitatu iliyopita.

  Taarifa hiyo imetolewa na Mwenyekiti wa Kamati ya Umoja wa Afrika Moussa Faki Mahamat hii leo mjini Addis Ababa, Ethiopia. Amesema maendeleo dhahiri yamefikiwa katika kutimiza uamuzi wa Mkutano Mkuu wa mwaka 2015 wa kuwa huru kifedha, na kusisitiza kuwa utekelezaji kamili wa Mfuko wa Amani wa Umoja wa Afrika kwa mwaka 2020 ni kipaumbele atakachokisimamia.

  Pia mwenyekiti huyo amesisitiza kuwa mchango wa kifedha kwa ajili ya Mfuko huo unatarajiwa kuongezeka hatua kwa hatua na kufikia dola za kimarekani milioni 400 mwaka ujao.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako