• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Ziara ya kwanza ya kila mwaka ya waziri wa mambo ya nje wa China barani Afrika yaonyesha hisia maalumu kati ya China na Afrika

  (GMT+08:00) 2020-01-14 18:59:10

  Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Bw. Geng Shuang leo amesema, ziara ya kwanza ya kila mwaka ya waziri wa mambo ya nje wa China barani Afrika ni kitendo cha kipekee, na imeonyesha hisia maalumu ya urafiki wa kizazi baada ya kizazi na kukabiliana na taabu kwa pamoja kati ya China na Afrika.

  Bw. Geng Shuang amesema katika ziara yake, Bw. Wang Yi na viongozi wa Afrika wamebadilishana maoni kuhusu kuimarisha uhusiano wa pande mbili na kuzidisha ushirikiano wa kunufaishana. Pande mbili zimeeleza kwamba, inapaswa kuharakisha utekelezaji wa matokeo yaliyofikiwa katika mkutano wa kilele wa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika uliofanyika Beijing, kuhimiza kwa sifa ya juu ushirikiano wa ujenzi wa "Ukanda Mmoja, Njia Moja", na kuzidisha ushirikiano katika sekta mbalimbali. Pia zimeona kuwa, kwa sasa uhusiano kati ya China na Afrika uko katika kipindi kizuri zaidi cha historia, ushirikiano kati ya pande hizo mbili una mustakabali mzuri, na utaendelea mbele ya ushirikiano kati ya nchi mbalimbali na Afrika.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako