• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Mazungumzo ya amani ya Libya hayakupata mafanikio

  (GMT+08:00) 2020-01-14 19:28:21

  Waziri wa mambo ya nje wa Russia Bw. Sergei Lavrov leo amesema hakuna makubaliano yaliyofikiwa kwenye mazungumzo ya amani ya Libya yaliyofanyika jana chini ya usuluhishi wa Russia na Uturuki, hata hivyo pande zote zitafanya juhudi kwa ajili ya kufikia makubaliano.

  Bw. Lavrov amesema, wataendeleza juhudi zaidi ili kutimiza lengo hilo, lakini hadi sasa hakuna matokeo yaliyofikiwa.

  Mapema mwezi huu, viongozi wa Russia na Uturuki walitoa pendekezo la kusimamisha vita nchini Libya, na pande zote za mapambano zilikubali pendekezo hilo na kukubali kufanya mazungumzo mjini Moscow.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako