• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Serikali ya Tanzania kuwaunga mkono wawekezaji

  (GMT+08:00) 2020-01-14 19:45:13
  Rais wa Jamhuri ya Tanzania John Magufuli,amesema kwamba serikali yake itawaunga mkono wafanyibiashara wazalendo wenye nia ya kuwekeza miradi ya maendeleo itakayokuza pato la taifa kiuchumi.

  Rais aliyasema hayo wakati akifungua hoteli ya Verde yenye hadhi ya nyota tano iliopo eneo la Mtoni, Unguja. Hoteli hii inamilikiwa na mtanzania, ambaye rais Magufuli alimsifu sana kwa kutumia fedha zake kuwanufaisha wananchi wazalendo kwa kuwekeza.#

  Rais alikemea tabia za baadhi ya watendaji serikalini kuwakatisha tamaa wafanyibiashara wazalendo. Magufuli aliwataka wafanyibiashara wa Tanzania kuwekeza kwanza nchini mwao kabla ya kuwekeza kwenye mataifa jirani.

  Aidha alitoa changamoto kwa taasisi zinazofanya kazi katika kutangaza utalii Zanzibar na Tanzania Bara, kushirikiana ili kuitangaza sekta hiyo. Alisema Tanzania Bara kwa mwaka imepokea watalii milioni 1.5, wakati Zanzibar ikipokea watalii 520,809 katika mwaka wa 2018.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako