• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Uganda: Serikali haijapata ombi la Kenya la kufutilia mbali ushuru kwa bidhaa zake

    (GMT+08:00) 2020-01-14 19:46:21
    Serikali ya Uganda imesema kwamba haijapokea ombi maalum kutoka kwa serikali ya Kenya la kufutilia mbali asilimi 13 ya ushuru unaotozwa kwa bidhaa zake zinaoingizwa nchini humo. Baadhi ya bidhaa hizi ni dawa, pombe na vileo.

    Akizungumza wikendi iliyopita, msemaji wa wizara ya Fedha Bwana Jim Mugunga, alisema kwamba serikali ya Uganda haina taarifa yoyote kuhusiana na ombi la kufutilia mbali ushuru.

    Wiki iliyopita, serikali ya Kenya kupitia katibu mkuu katika wizara ya Biashara bwana Chris Kiptoo, ilisema kwamba kufuatia mazungumzo ya Desemba mwaka uliopita jijini Kampala kati ya mataifa haya mawili, serikali ya Uganda ilichukuwa hatua ya kufutilia mbali ushuru wa asilimia 13 ambayo imekuwa ikitoza kwa dawa, pombe na vileo kutoka Kenya. Hatua hii ilikuwa njia moja ya kuhakikisha kwamba kuna usawa katika kufanyabiashara ya kuagiza bidhaa katia ya Kenya na Uganda.

    Hta hivyo endapo Uganda haitafutilia ushuru huu, basi Kenya italazimika mkutoza ushuru uo huo kwa bidhaa za Uganda zinazoingia nchini Kenya.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako