• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Sudan: Fedha za mafuta kutumiwa kwenye kilimo

  (GMT+08:00) 2020-01-14 19:54:48

  Serikali ya Sudan imechukuwa hatua ya kufufua sekta ya kilimo kwa kutumia fedha zitakazopatikana kwa kuuza mafuta yake kwa mataifa mengine. Mpango huu uliotangazwa na rais Salva Kiir, unalenga kumaliza tatizo la njaa nchini Sudan na kuacha kutegemea chakula cha misaada kutoka nje.

  Sekta ya kilimo nchini Sudan imekumbwa na ugumu kuanzia mwaka wa 2013 baada ya vita vya kisiasa.

  Waziri wa Kilimo Bwana Onyoti Adigo anasema kwamba kupitia fedha za mafuta, serikali itasambaza pembejeo kwa raia wake kwa bei ya chini, hii ni katika awamu ya majaribio ya kufufua kilimo nchini humo.

  Kulingana na bei ya sasa ya mafuta, serikali ya Sudan inapokea zaidi ya dola milioni 5.5 kwa siku au zaidi ya dola milioni 165 kila mwezi. Tangazo la Rais Salva Kiir la kukumbatia kilimo linajirimajuma kadhaa baada ya shirika la World Food Programme kusema kwamba huenda Sudan Kusini ikakumbwa na njaa siku 30 zijazo endapo misaada haitakuwepo.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako