• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Nchi za SADC kutekeleza mfumo wa kutumia kwa pamoja satelaiti

  (GMT+08:00) 2020-01-14 20:05:03

  Waziri wa Mawasiliano ya Simu nchini Angola, Mario Oliveira amesema, utekelezaji wa mfumo wa kutumia kwa pamoja satelaiti utasaidia kuboresha maendeleo endelevu katika bara la Afrika.

  Akizungumza katika semina ya Jumuiya na Kiuchumi ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC) iliyofanyika mjini Luanda, Oliveira amesema mfumo huo utawezesha watu wa Afrika kupata kwa urahisi taarifa, na kuongeza kuwa itakuwa ni hatua muhimu kwa nchi wanachama wa SADC kuingia kwenye sekta ya anga za juu.

  Naye mratibu wa ngazi ya juu wa sayansi, teknolojia na mawasiliano wa SADC Geoge Ah-Thew amesema, nchi wanachama wa Jumuiya hiyo zinaandaa sera kwa ajili ya mfumo huo.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako