• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Iran yakaribisha hatua yoyote ya kuokoa makubaliano ya nyuklia

    (GMT+08:00) 2020-01-15 11:11:33

    Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya Iran Bw. Abbas Mousavi amesema Iran inakaribisha hatua yoyote ya kiujenzi ya kuokoa makubaliano yaliyofikiwa mwaka 2015 kuhusu suala la nyuklia JCPOA.

    Msemaji huyo amesema Iran iko tayari kupokea hatua yoyote yenye nia njema na ya kiujenzi ya kuokoa makubaliano hayo muhimu ya kimataifa, na wakati huohuo imefahamisha pande husika haswa nchi tatu za Ulaya, kwamba kitendo chochote cha kukiuka ahadi, nia mbaya na hatua zisizo za kiujenzi zitajibiwa na Iran.

    Bw. Mousavi ameyasema hayo kufuatia Uingereza, Ufaransa na Ujerumani kutangaza kuanzisha utaratibu wa kushughulikia migogoro kwa mujibu wa makubaliano ya JCPOA.

    Taarifa ya pamoja iliyotolewa na nchi hizo inasema, madhumuni ya kuanzishwa kwa utaratibu huo ni kuhimiza Iran kufuata tena kikamilifu ahadi zake kwenye makubaliano hayo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako