• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • SOKA: Jose Mourinho asema hajafanya mazungumzo yoyote ya uhamisho wa Victor Wanyama

  (GMT+08:00) 2020-01-15 14:10:07

  Meneja wa Tottenham Hotspur, Jose Mourinho, amebainisha kuwa hajafanya mazungumzo yoyote ya uhamisho wa Victor Wanyama huku ripoti zikiibuka kuwa ataondoka klabu hiyo. Wanyama hajashirikishwa katika kikosi chochote tangu Mourinho alipomrithi Mauricio Pochettino kama kocha wa Spurs mnamo Novemba mwaka jana. Kiranja huyo wa Kenya, ameshirikishwa katika mechi moja pekee chini ya uongozi wa Mourinho, kama mchezaji wa akiba ambapo Tottenham ilipoteza 3-1 kwa Bayern Munich katika Mabingwa wa Ligi. Kocha huyo wa zamani wa Southampton kwa sasa anakumbana na hatma finyu katika klabu hiyo ya Uingereza huku duru zikiarifu kuwa huenda akaondoka kabla ya kutamatika kwa mkataba wake na Spurs. Akizungumza katika kikao na wanahabari, Mourinho alikiri kwamba hajawahi jadiliana na Mkenya huyo kuhusiana na hatma yake na Spurs. Licha ya Mourinho kumsifu, Wanyama anaonekana kuwa huru kuondoka Spurs ili kufufua taaluma yake. Hata hivyo staa huyo wa zamani wa Celtic ameanza kumezewa mate na vilabu vya Ulaya, vikiwemo Galatasaray na Hertha Berlin ambavyo vinatamani huduma yake.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako