• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • SAKATA: Bilionea Mohamed 'Mo' Dewji ameza kauli yake ya kujiuzulu Simba

    (GMT+08:00) 2020-01-15 14:10:31

    Lile sakata la Bilionea Mohamed 'Mo' Dewji kujiuzulu Uenyekiti wa Bodi ya Ukurugenzi ya Simba sasa limechukua sura mpya baada ya bilionea huyo jana kumeza kauli yake hiyo ya kujiuzulu. Baada ya Simba kuchapwa 1-0 na Mtibwa Sugar katika fainali ya Kombe la Mapinduzi Uwanja wa Amaan, Zanzbar Dewji juzi alitangaza kujiuzulu kupitia ukurasa wake wa Twitter. Lakini jana baada ya kikao hicho akaikana Tweet hiyo akisema haelewi kilichotokea kwenye akaunti yake na kuwahakikishia wana Simba kwamba bado yuko nao bega kwa bega na sasa anaelekeza nguvu kwenye Ligi Kuu, pia kaipongeza timu ya Mtibwa kwa kuchukua kombe.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako