• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • SOKA: City Stars yazidi kutetemesha BNSL

  (GMT+08:00) 2020-01-15 16:28:50

  Wanasoka wa Nairobi City Stars waliendelea kufyeka wapinzani wao kwenye kampeni za kuwania taji la Betika Supa Ligi ya Taifa (BNSL) walipowafunga Shabana FC bao 1-0 uwanjani Gusii mjini Kisii. Nayo Bidco United ilikandamiza Mt Kenya United kwa magoli 5-2 na kuendelea kubaki katika nafasi ya pili kwenye jedwali kwa alama 39 huku Muranga Seal ikifungwa bao 2-1 mbele ya Kibera Black Stars. City Stars ambayo iko chini ya kocha Sanjin Alagin ilipata mtihani mgumu mbele ya wenyeji wao kabla ya Abdallah 'Shittu' Salim kufanya kweli. Mshambuliaji huyo alifanikiwa kutikisa wavu mara moja na kubeba City Stars kutia kapuni alama tatu muhimu.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako