• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • SOKA: Mwanasoka atia saini kucheza hadi umri wa miaka 53

  (GMT+08:00) 2020-01-15 16:29:24

  Msakataji mzee wa kabumbu duniani Kazuyoshi Miura amesaini mkataba mpya utakaoshuhudia akiendelea kuvalia daluga zake hadi atakapofikisha umri wa miaka 53. Miura ni mshambuliaji wa kati kutoka Japan ambaye alizaliwa Februari 26 mwaka 1967 mjini Shizuoka. Vyombo vya habari nchini Uingereza vimeripoti kuwa Januari 13, 2020 Miura, ambaye amekuwa akisakata soka kwa miaka 34, amesaini kandarasi ya mwaka mmoja na Yokohama FC. Klabu ya Yokohama itashiriki Ligi Kuu nchini Japan mwaka 2020 baada ya kupata tiketi kwa kumaliza Ligi ya Daraja ya Pili katika nafasi ya pili nyuma ya Kashiwa Reysol anayochezea Mkenya Michael Olunga mwaka 2019.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako