• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • SOKA: Yanga yasajili mshambuliaji Mghana

  (GMT+08:00) 2020-01-15 16:31:03

  Klabu ya Yanga Sc imetangaza usajili wa mchezaji raia wa Ghana, Bernard Morrison mwenye umri wa miaka 26, kutoka klabu ya DC Motema Pembe ya nchini DRC Congo. Takwimu za Morrison: Ligi kuu Afrika Kusini amecheza michezo 18 na kufunga mabao mawili, ligi kuu Ghana katika michezo 16 ametikisa nyavu mara 6. Mchezaji huyo anamudu kucheza nafasi mbalimbali uwanjani katika safu ya ushambuliaji, mshambuliaji wa kati na mshambuliaji wa pembeni akitokea kulia ama kushoto. Bernard amewahi kuchezea timu kadhaa kabla ya kutua Jangwani katika dirisha hili dogo la usajili, amepita As Vita, Dc Motema Pembe, Ashanti ya Ghana na Orlando Pirates ya Afrika Kusini.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako