• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Uchaguzi wa Taiwan hauwezi kubadilisha ukweli kwamba Taiwan ni sehemu ya ardhi ya China

  (GMT+08:00) 2020-01-15 17:11:39

  Msemaji wa Ofisi ya mambo ya mkoa wa Taiwan ya Baraza la Serikali la China Bw. Ma Xiaoguang amesema, uchaguzi uliofanyika mkoani Taiwan hauwezi kubadilisha ukweli kwamba Taiwan ni sehemu ya ardhi ya China.

  Bw. Ma amesisitiza kuwa, bila ya kujali matokeo ya uchaguzi huo, sera na mwongozo wa serikali kuu kuhusu mambo ya Taiwan haitabadilika, na bila ya kujali hali ya siasa ya Taiwan itapata mabadiliko gani, maendeleo ya amani ya uhusiano kati ya kando mbili za Mlango Bahari wa Taiwan yataendelea kuwa matumaini ya wakazi wa mkoani Taiwan. Amesema kushikilia "Makubaliano ya mwaka 1992" yanayoonesha "kanuni ya kuwepo kwa China moja" kutahimiza uhusiano kati ya pande hizo mbili kuboreshwa na kuendelezwa, na maslahi ya wakazi wa Taiwan yatahakikishwa. Ameongeza kuwa, bila ya hivyo, uhusiano kati ya pande hizo mbili utaharibiwa, hali ya kando mbili za Mlango Bahari wa Taiwan itakabiliwa na migogoro, na maslahi za wakazi wa Taiwan pia yataathiriwa.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako