• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Jeshi la Sudan ladhibiti tena majengo ya idara za usalama

    (GMT+08:00) 2020-01-15 17:32:08

    Mwenyekiti wa Baraza la Pamoja la Utawala nchini Sudan Abel Fattah al-Burhan amesema, vikosi vya serikali vimedhibiti tena majengo yote ya Idara Kuu ya Upelelezi (GIS) ambayo yalitekwa Jumanne na makundi ya waasi.

    Akizungumza na waandishi wa habari mapema leo, Al-Burhan amesema majengo yote yamedhibitiwa tena na jeshi la serikali. Pia kiongozi huyo alitangaza kufunguliwa kwa anga ya Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Khartoum, ambao ulifungwa na mamlaka kwa saa tano kama hatua ya tahadhari.

    Amesisitiza kuwa jeshi la Sudan limedhamiria kukabiliana na jaribio lolote la kuharibu usalama, na kuahidi kuwa jeshi hilo litalinda mabadiliko na halitoruhusu mapinduzi yoyote.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako