• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Waziri wa mambo ya nje wa China akutana na mwenzake wa Kenya

    (GMT+08:00) 2020-01-15 17:40:55

    Waziri wa mambo ya nje wa China Bw. Wang Yi ambaye yuko ziarani barani Afrika, Ijumaa iliyopita alikutana na mwenzake wa Kenya Bibi Monica Juma mjini Mombasa.

    Kwenye mazungumzo yao, Bibi Juma alisema Kenya inapenda kushirikiana na China katika kutekeleza kwa makini makubaliano yaliyofikiliwa na viongozi wa nchi hizo mbili, na kupanua na kuimarisha ushirikiano wa kiutendaji, kuharakisha ujenzi wa pamoja wa "Ukanda Mmoja, Njia Moja". Ameongeza kuwa reli ya SGR ni mradi wa kunufaishana, ambayo uendeshaji wake unaendelea vizuri kwa ufanisi, na imekuwa njia muhimu zaidi ya uchukuzi nchini Kenya. Ameishukuru China kwa kuunga mkono maendeleo ya kiuchumi na kijamii ya Kenya, na kuisifu China kwa kufanya juhudi za kiujenzi katika kuhimiza amani na maendeleo ya Afrika.

    Kwa upande wake, Wang Yi alisema China inapenda kuimarisha ushirikiano wa kunufaishana na Kenya kwenye sekta mbalimbali, ikiwa ni pamoja na kuongeza bidhaa za kilimo za Kenya zinazouzwa kwenye soko la China. Amesema China inapenda kutumia jukwaa la Baraza la Ushirikiano wa China na Afrika na kukutoa mchango wake juu ya maendeleo endelevu na usalama wa nchi zote za Afrika ikiwemo Kenya.

    Wang Yi alikagua reli ya SGR kufahamu ujenzi na uendeshaji wake.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako