• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kongamano la kukuza mawasiliano ya tasnia ya ubunifu na utamaduni lafanyika nchini Rwanda

    (GMT+08:00) 2020-01-15 18:51:27

    Kongamano lililoandaliwa na Times Multimedia, Benki ya Usafirishaji ya Afrika (Afreximbank) na serikali ya Rwanda litafanyika Ijumaa na Jumamosi wiki hii mjini Kigali.

    Watu 1,500 watahudhuria kongamano hilo linalohusu mawasiliano ya tasnia ya ubunifu, na kuonyesha vipaji vya ubunifu kutoka sekta ya muziki, sanaa na mitindo.

    Mkuu wa idara ya utalii chini ya Bodi ya maendeleo ya Rwanda Bw. Belise Akariza amesema, tasnia ya ubunifu ni sehemu muhimu ya maendeleo ya uchumi na kuunda ajira, haswa kwa vijana.

    Naye meneja wa ofisi ya mpango na biashara ya ndani wa Afreximbank Bw. Temwa Gondwe amesema, bidhaa za tasnia ya ubunifu ni muhimu sana katika kumaliza tatizo la ajira kwa vijana na kukuza uvumbuzi, na wanachunguza njia za kuvumbua tasnia mpya.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako