• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • China yasikitishwa na kuanzishwa kwa utaratibu wa kutatua mgogoro juu ya makubaliano ya suala la nyuklia la Iran

  (GMT+08:00) 2020-01-15 19:12:27

  Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Bw. Geng Shuang leo amesema China imesikitishwa na hatua ya Uingereza, Ufaransa na Ujerumani kuanzisha utaratibu wa kutatua mgogoro juu ya makubaliano ya suala la nyuklia la Iran.

  Amesema, kitendo hicho hakitasaidia kutatua mgogoro, pia hakitasaidia kupunguza hali ya sasa ya wasiwasi. Amesema China siku zote inaona kuwa, Iran ina sababu zake za kupunguza utekelezaji wake wa makubaliano hayo. Sababu ya hali ya wasiwasi kuhusu suala la nyuklia la Iran ni kitendo cha Marekani kujitoa kutoka makubaliano hayo, kupuuza sheria ya kimataifa na majukumu ya kimataifa, kushikiniza Iran na kuweka vikwazo kwa Iran kutekeleza makubaliano hayo.

  Bw. Geng Shuang pia amesema, China itaendelea kuwasiliana na pande husika, kuhimiza suala la nyuklia la Iran kutatuliwa kwa njia ya mazungumzo na ya kisiasa, kutoa mchango kwa ajili ya kulinda makubaliano ya suala la nyuklia la Iran na kupunguza hali ya wasiwasi katika Mashariki ya Kati.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako