• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China kuendelea kupanua uagizaji wa bidhaa kutoka nje

    (GMT+08:00) 2020-01-15 19:14:36

    Mkurugenzi wa Idara ya biashara ya nje kwenye Wizara ya biashara ya China Bw. Li Xingqian amesema, mwaka 2019 biashara ya nje ya China ilipata maendeleo wakati uchumi wa dunia ukikabiliana na changamoto mbalimbali. Amesema mwaka 2020 sekta hiyo ya China itadumisha maendeleo wenye utulivu, na China itapanua uagizaji wa bidhaa kutoka nje, ili kuchangia ufufukaji wa uchumi duniani na ongezeko la biashara.

    Takwimu kutoka Idara kuu ya forodha ya China zimeonesha kuwa, mwaka 2019 thamani ya jumla ya uagizaji wa bidhaa na mauzo ya bidhaa nje ya China kwa mwaka mzima ilikuwa dola za kimarekani trilioni 4.6, likiwa ni ongezeko la asilimia 3.4. Mkurugenzi wa biashara ya nje kwenye Wizara ya Biashara ya China Bw. Li Xingqian ameeleza kuwa, thamani ya uuzaji wa bidhaa nje ya China inachukua nafasi kubwa zaidi katika masoko ya kimataifa, huku thamani ya uagizaji wa bidhaa kutoka nje ikichukua zaidi ya asilimia 10 katika thamani ya jumla ya uagizaji wa bidhaa duniani.

    "China imekuwa ikipanua soko kwa dunia, na kudumisha kuwa soko la pili kwa uagizaji wa bidhaa kwa wingi zaidi kutoka nje kwa miaka 11 mfululizo. Tangu mgogoro wa fedha duniani ulipotokea, uagizaji wa bidhaa wa China kutoka nje umechangia moja ya sita ya thamani ya jumla ya uagizaji wa bidhaa duniani, na imekuwa chombo cha kuhimiza ufufukaji wa uchumi duniani."

    Bw. Li Xingqian pia ameeleza kuwa, hadi sasa China imekuwa mwenzi muhimu wa biashara kwa nchi na sehemu zaidi ya 120 duniani. Akizungumzia hali ya biashara ya nje katika mwaka 2020, Bw. Li anasema:

    "Hivi sasa maendeleo ya biashara ya nje yanakabiliwa na hali ngumu zaidi, na ongezeko la uchumi na biashara la dunia linapungua. Wakati huo huo serikali ya China inatekeleza kwa hatua madhubuti ufunguaji mlango wenye kiwango cha juu, maendeleo ya biashara ya nje yana msingi imara, uwezo wa viwanda vya kufanya uvumbuzi na kupanua soko pia umeongezeka kwa udhahiri. Tuna imani kudumisha maendeleo ya biashara ya nje kupata maendeleo kwa utulivu."

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako