• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Wataka kampuni ya mawe ifungwe

  (GMT+08:00) 2020-01-15 20:48:04
  Zaidi ya wakazi 500 katika kaunti ya Thika wameitaka serikali kufanya mazungumzo na kampuni ya China inayojihusisha na shughuli ya usagaji mawe ili kuona ni jinsi gani wanaweza kuzuia vumbi na kuruka kwa mawe wakati wa shughuli zao. Wakazi hao wameitaka kampuni ya Sinohydro Corporation ambayo ni ya kichina kufanya mazungumzo ya mara kwa mara kuona ni jinsi gani wanaweza kuzuia halia hiyo. Kampuni hiyo ya Sinohydro Corporation husaga mawe ambayo hugeuzwa kama kokoto ya kujenga nyumba na kazi hiyo huendeshwa masaa 24 mfululizo.

  Wengi wao walisema pindi watakapofanya mazungumzo na pande husika wanaweza kutatua hali hiyo haraka iwezekana. Wakati huo huo hofu ya njaa imezuka katika eneo la kati nchini Kenya kufuatia wasiwasi kwamba nzige wanaoenea Kenya huenda wakaharibu mazao ya mahindi, mpunga, majani chai na kahawa. Tayari nzige hao wamevamia mashamba ya katika baadhi ya maeneo nchini Kenya.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako