• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Tanzania yatakiwa kuwafikia watalii wa China kwa kutumia majukwaa mitandaoni

  (GMT+08:00) 2020-01-15 20:48:29

  Balozi wa Tanzania nchini China Bwana Mbelwa Kairuki amesema kuna haja kubwa kwa Tanzania kuwasiliana na wenzao wa China kwa kutumia mitandao ya kijamii ili kupiga jeki sekta ya utalii nchini humo. Kairuki amesema ubalozi wa Tanzania nchini China hivi sasa unafungua jukwaa la mtandao ili kuuza vivutio vya utalii vya Tanzania . Amesema jukwaa hilo litakuwa linaitangaza Tanzania kwa wachina na wadau wa utalii ambao wangependa kutangaza huduma zao kwa wachina kupitia jukwaa hilo watalazimika kulipia kwa muda wa miezi sita.

  China imepiga hatua kubwa sana katika mambo ya technolojia na baadhi ya mitandao ya kijamii inayowavutia wachina zaidi ni Wechat, weibo na QQ. Tanzania na China wamekuwa wakishirikiana kwa mambo mengi tu ya kibiashara hususan wakati huu ambapo Tanzania inalenga kupata ufanisi mkubwa kwenye uchumi wa kiviwanda.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako