• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Sudan Kusini yatangaza tenda ya kukagua madhara ya hali ya kimazingira katika maeneo ya visima vya mafuta

    (GMT+08:00) 2020-01-15 20:48:59

    Sudan Kusini imetangaza tenda ya kukagua mazingira ya visima vyote vya mafuta nchini humo kabla shughuli ya uchimbaji mafuta kuannza. Ukaguzi huo unaendana na matakwa ya sheria ya mafuta ya mwaka wa 2012 ambayo pia inasimamia sekta ya mafuta nchini humo. Aidha sheria hiyo imeundwa kwa ajili ya kufanikisha usimamizi wa hali ya mazingira inayotokana na shughuli za uchimbaji mafuta. Inasemekana kampuni moja ya kimataifa ndio itakayopewa kandarasi hiyo na itatakiwa kutoa mapendekezo kuhusu maeneo ambayo yanatakiwa kuchimbwa kwa ajili ya kutafuta mafuta pamoja na kurekebisha uharibifu ambao umefanywa kutokana na shughuli za uchimbaji mafuta na gesi.

    Waziri wa mafuta wa Sudana Kusini Bwana Daniel Chuang uharibifu unaotokana na moshi mbaya utaiwezesha nchi hiyo kuweka mikakati ili kuzuia madhara zaidi kutokea.

    Mwaka jana, rais Salvar Kiir amesema serikali yake itachukua msimamo mkali dhidi ya uchafuzi wa mazingira unaoshuhudiwa katika maeneo ambayo shughuli za uchimbaji madini zinaendelea.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako