• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Tanzania yaitaji uniti 10,000 kwa viwanda

  (GMT+08:00) 2020-01-15 20:49:24
  Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) limesema jumla ya Uniti 10,000 zinahitajika ili kufikia Tanzania ya viwanda. Mkurugenzi wa Tanesco Dk. Tito Mwinuka amesema Tanesco imejipanga kimkakati ili kufanikisha azma hiyo ya serikali.

  Aliyasema hayo jana alipofungua mafunzo elekezi kwa baadhi ya wafanyakazi wapya wa shirika hilo, akibainisha kuwa liliajiri watumishi wapya 958 hivi karibuni.

  Mkuu wa Chuo cha Utumishi wa Umma, Dk. Emmanuel Shindika, aliwataka wafanyakazi hao wapya kuhakikisha wanasimamia maadili waliyofundishwa ili kufanya kazi kwa uadilifu.

  Alisema hakuna sababu ya kupindisha sheria zilizowekwa kazini, badala yake kuzifuata kama maadili ya utumishi wa umma yanavyoelekeza.

  Wengi wa wafanya kazi hao wamesema tayari wamefundishwa kila kitu walichostahili hivyo basi wanapaswa kutendea haki na si kubweteka.

  Wafanyakazi wamepewa mafunzo elekezi ya siku sita kabla ya kuanza kazi ili kwenda sambamba na kasi ya shirika hilo katika utendaji wao.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako