• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mwakilishi wa China aitaka serikali ya Mali ifanye juhudi kwa ajili ya amani na maendeleo

    (GMT+08:00) 2020-01-16 09:10:42

    Naibu mwakilishi wa kudumu wa China kwenye Umoja wa Mataifa balozi Wu Haitao ameitaka serikali ya Mali ifanye juhudi kuhimiza amani, maendeleo ya uchumi na ushirikiano wa kikanda.

    Balozi Wu amesema serikali ya Mali na pande nyingine husika lazima zichukue hatua ili kushughulikia hali dhaifu ya usalama, vurugu za kikabila, hali mbaya ya kibinadamu na ugaidi.

    Kwenye mkutano wa Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa, balozi Wu ameitaka serikali ya Mali ifanye mazungumzo na pande nyingine husika, ili kutatua migongano kwa njia ya amani, na kuhimiza mchakato wa amani na kufanya juhudi kwa pamoja kwa ajili ya amani na maendeleo ya taifa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako