• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wizara ya mambo ya nje ya China yaitarajia Uingereza ijiamulie mambo kulingana na maslahi yake

    (GMT+08:00) 2020-01-16 10:25:45

    Kufuatia Marekani kutoa shinikizo kwa Uingereza kupiga marufuku kutumia teknolojia ya 5G ya kampuni ya Huawei ya China, msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Bw. Geng Shuang amesema, anatarajia Uingereza itatoa uamuzi wake kwa uhuru na haki kulingana na maslahi yake na kuipa kampuni ya China mazingira yenye haki, usawa, uwazi na bila upendeleo.

    Bw. Geng amesema, kampuni ya Huawei imefanya biashara kwa miaka mingi, na kuwekeza mamilioni ya paundi, kutoa maelfu ya nafasi za ajira, kujenga taasisi ya muungano na kutekeleza majukumu ya kijamii nchini humo.

    Bw. Geng pia meitaka Marekani kuacha kuilaani ovyo China katika sekta ya usalama bila ya ushahidi na kukandamiza makampuni ya China.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako