• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • KIKAPU: Morans yawaliza Tanzania kwa vikapu 95-55

    (GMT+08:00) 2020-01-16 12:33:22

    Timu ya mpira wa kikapu ya Kenya Morans, jana iliwaliza Tanzania kwa vikapu 95-55 kwenye michuano ya kabla ya mechi za kufuzu Fiba Afro basketball ambapo mashindano hayo jana yaliingia siku ya pili kwenye uwanja wa Taifa wa Nyayo Gymnasium. Kocha wa Kenya Cliff Owuor amesema jana walifanya vizuri kuliko juzi kwasababu wachezaji walicheza kwa mshikamano na kushambulia Zaidi. Naye kocha wa Tanzania Alfred Ngalaliji amelaumu kutokuwepo kwa wachezaji wake muhimu ndio kumepelekea kushindwa kwa timu. Amesema wachezaji wake wengi ni wanajeshi ambao walikuwa likizo na ilikuwa vigumu kuwaita kushiriki kwenye michuano hiyo. Mapema siku hiyo, Sudan Kusini iliendelea kuiaibisha Eritrea kwa vikapu 111-57 baada ya kuongoza kwa 63-23 wakati wa mapumziko huku Burundi ikiihakikishia Somalia inaondoka patupu baada ya kuichabanga vikapu 104-86.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako