• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Rais wa China atoa makala kwenye magazeti ya Myanmar

  (GMT+08:00) 2020-01-16 16:54:24

  Rais Xi Jinping wa China leo ametoa makala kwenye magazeti ya Myanmar Alin Daily, Global New Light of Myanmar na Kyemon.

  Katika Makala hizo, Rais Xi amesema China inapenda kushirikiana Myanmar kusukuma mbele kujenga jumuiya yenye mustakabali wa pamoja yenye ukaribu zaidi kati ya China na Myanmar, na kuendeleza urafiki uliodumu kwa miongo kadhaa.

  Kwenye makala hiyo iliyoitwa "kuandika ukurasa mpya wa urafiki wa ndugu unaodumisha miaka ya maelfu", rais Xi amesema katika miaka 70 iliyopita tangu China na Myanmar kuanzisha uhusiano wa kibalozi, nchi hizo zimetekeleza kanuni tano za kuishi kwa amani, kuaminiana, kuheshimiana, kuungana mkono na kutoa mfano mzuri wa nchi kubwa na ndogo kutendeana kwa usawa, kunufaishana na kujiendeleza kwa pamoja, pia kuleta manufaa halisi kwa watu wa nchi hizo mbili.

  Rais Xi pia amesema pande hizo mbili zinapaswa kutumia fursa hii ya kuadhimisha miaka 70 tangu nchi hizo kuanzisha uhusiano wa kibalozi, kuimarisha zaidi mawasiliano ya kimkakati, kuzidisha biashara, kupanua maingiliano, na kuongeza uratibu na ushirikiano katika mambo ya kikanda na kimataifa, ili kuhimiza uhusiano kati ya China na Myanmar kuingia kwenye kipindi kipya.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako