Gavana wa Kirinyaga Anne Waiguru ameanzisha mazungumzo kati ya serikali yake na wawekezaji wa India ambao wameelezea nia ya kununua kahawa.
Vile vile, amekuwa akifanya mazungumzo na wasimamizi wa vyama 15 vya ushirika kutoka eneo la Mlima Kenya kwa lengo la kuimarisha bei ya zao.
Wawekezaji hao kutoka India ambao ni wanachama wa kampuni ya SPG group of Companies, watarajiwa kuanza kununua kahawa baada ya makubaliano kuafikiwa.
Gavana Waiguru alifafanua kuwa serikali yake itahakikisha wakulima wanauza kahawa yao kwa mkataba wa miaka 10 ambapo watahakikishiwa mapato ya kudumu.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |