• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Tanzania: Shilingi bilioni 35 zapatikana kutoka kwa mauzo ya madini

  (GMT+08:00) 2020-01-16 19:34:38

  Madini ya Sh34.5 bilioni yameuzwa katika soko la madini mjini Arusha kuanzia Januari hadi Desemba 2019.

  Hayo yameelezwa na naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo na kubainisha kuwa kati ya fedha hizo, Serikali imepata mrabaha wa Sh1.2 bilioni na Sh350 milioni za ada ya ukaguzi.

  Nyongo alieleza hayo wakati akifungua mkutano uliomhusisha balozi wa China nchini Tanzania, balozi wa Tanzania nchini China, wafanyabiashara na wachimbaji wa madini kujadili fursa za kupata masoko ya madini China.

  Nyongo amesema katika soko la dhahabu wilayani Karatu, madini ya Sh198 .5 milioni yameuzwa.

  Amesema kati ya fedha hizo, Serikali umepata mrabaha wa Sh11.9 milioni na Sh1.6 milioni za ada ya ukaguzi.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako