• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Rwanda: Kiwanda cha maziwa cha Burera chauzwa kwa mwekezaji wa Zimbabwe

  (GMT+08:00) 2020-01-16 19:36:00
  Serikali ya Rwanda imeuza kiwanda cha maziwa cha Burera kwa mwekezaji wa Zimbabwe.

  Kiwanda hicho kilimilikiwa kwa asilimia 98.3 na serikali na ilitangaza mipango ya kukiuza mwezi Disemba mwaka jana.

  Kilianzishwa mwaka 2016 kwa gharama ya franc milioni 488 ili kusaidia wafugaji wa ngombe wa maziwa kwenye eneo la Burera.

  Kampuni ya Afrisol ya Zimbabwe ilionunua kiwanda hicho imesema inapanga kuongeza usindikaji wa maziwa na kutoa mafunzo kwa wakulima kuhusu njia za kisasa za ufugaji ili kuongeza uzalishaji.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako