• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Zanzibar: Wajasiriamali watakiwa kuzalisha bidhaa zenye ubora

  (GMT+08:00) 2020-01-16 19:37:12

  Mkurugenzi wa Taasisi ya Ubora na Viwango Zanzibar (ZBS), Khatib Mwadini, amewataka wafanyabiashara kuhakikisha wanazalisha bidhaa zenye ubora ili kunusuru afya za wananchi.

  Akizungumza na wananchi na wafanyabiashara katika Maonyesho ya Biashara ya Miaka 56 ya Mapinduzi huko Maisara mjini Zanzibar, alisema iwapo watazalisha bidhaa zenye ubora, zitakuwa na ushindani mkubwa wa soko la ndani na nje.

  Mwadini alisema taasisi hiyo itahakikisha afya za watumiaji wa bidhaa zinakuwa salama na kuwachukulia hatua za kisheria wafanyabiashara.

  Pia alisema watahakikisha wanalinda usalama wa afya za wananchi ili kuimarisha uchumi wa nchi na kwamba afya zikiimarika watafanya kazi zao kwa ufanisi.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako