• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Uganda yapinga maziwa yanayotoka nchini humo kukamatwa Kenya

    (GMT+08:00) 2020-01-16 19:57:19

    Serikali ya Uganda imeilalamikia nchi jirani ya Kenya kwa kile ilichoita kukamatwa kwa bidhaa za maziwa kutoka Uganda.

    Msemaji wa serikali ya Uganda Ofwono Opondo amesema, wizara ya mambo ya nje iliandika barua hapo jana ikieleza wasiwasi wake kutokana na kukamatwa isivyo halali kwa bidhaa za maziwa zilizotoka nchini Uganda chini ya chapa ya Lato, hatua iliyosababisha hasara kubwa kwa kampuni hiyo. Wizara hiyo imesema, kuanzia Januari 2 bidhaa zenye thamani ya dola za kimarekani 360,000 zimekamatwa.

    Uganda imesema, hatua hiyo ni kinyume na kanuni ya ujirani mwema na wajibu wa Kenya chini ya mkataba ulioanzisha Jumuiya ya Afrika Mashariki, Itifaki ya Umoja wa Forodha, Itifaki ya Soko la Pamoja, na makubaliano ya uwezeshaji wa kibiashara ya Shirika la Biashara Duniani.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako