• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wanauchumi wa Marekani wasema kusainiwa kwa makubaliano ya biashara ya kipindi cha kwanza kati ya China na Marekani kutachangia uchumi wa dunia

    (GMT+08:00) 2020-01-16 20:02:03

    Hafla ya kusainiwa kwa makubaliano ya biashara ya kipindi cha kwanza kati ya China na Marekani imefanyika rasmi kwenye Ikulu ya Marekani. Rais Donald Trump wa Marekani na Naibu waziri mkuu wa China ambaye pia ni kiongozi wa ujumbe wa China kwenye mazungumzo hayo Bw. Liu He wamesaini makubaliano hayo mjini Washington.

    Kusainiwa kwa makubaliano hayo kumepongezwa sana na sekta ya biashara nchini Marekani, ikiamini kuwa yatanufaisha pande zote mbili za China na Marekani. Baadhi ya wanauchumi wanaona kuwa, kusainiwa kwa makubaliano hayo kutachangia uchumi wa kikanda, uchumi kati ya China na Marekani na ule wa dunia.

    Mwanauchumi wa Marekani Bw. David Paul Goldman anaona kuwa, kusainiwa kwa makubaliano hayo kunasaidia kupunguza migogoro ya biashara kati ya China na Marekani, na pia kutachochea ukuaji wa uchumi duniani.

    "Naona kuwa hali isiyotabirika itapungua, na itaboresha mambo ya uwekezaji. Viwanda na utengenezaji vitaweza kufufuka hatua kwa hatua nchini Marekani. Vilevile itachochea nchi zinazotegemea zaidi uuzaji wa bidhaa nje ya nchi zikiwemo Ujerumani, Japan na Korea Kusini."

    Mkuu wa Kamati ya kitaifa ya biashara kati ya Marekani na China Bw. Craig Allen anaona kuwa, kusainiwa kwa makubaliano hayo si kama tu kunawanufaisha watu wa Marekani na China, vilevile kutachangia maendeleo ya dunia.

    "Tunafurahia kusainiwa kwa makubaliano hayo. Linalonifurahisha zaidi ni kwamba pande zote mbili za Marekani na China zitanufaika kutokana na makubaliano hayo."

    Mkuu wa mtaa wa Brooklyn wa mji wa New York wa Marekani Bw. Eric Adams anaona kuwa, kusainiwa kwa makubaliano hayo ni hatua ya kwanza kwa China na Marekani kurejesha uhusiano wa kawaida wa wenzi wa uchumi na biashara.

    "Endapo migogoro ya biashara itamalizika, itanufaisha pande zote mbili, China na Marekani. Na ikidumishwa hakutakuwa na upande utakaoshinda. Tunaamini kuwa migogoro hiyo itamalizwa, na tutaweza kuwa tena wenzi wazuri wa biashara."

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako