• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • KIKAPU: Tanzania yaipa darasa Eritrea kwenye michuano ya kabla ya mechi za kufuzu ya Fiba Afro basketball

    (GMT+08:00) 2020-01-17 09:51:19

    Tanzania imeipa kibano kikali Eritrea cha vikapu 101-69 katika mechi yao ya pili kwenye michuano ya kabla ya mechi za kufuzu ya Fiba Afro basketball iliyoendelea jana katika uwanja wa Taifa wa Nyayo. Tanzania, ambao wameandikisha wachezaji sita tu katika michuano hii bada ya wachezaji wengine wa timu kushindwa kushiriki katika dakika za mwisho walianza kuongoza mapema kwa 23-19 katika robo ya kwanza na kuongeza 51-38 hadi kufikia mapumziko. Katika mechi nyingine ya jana Sudan Kusini nao walikuwa na kibarua chepesi dhidi ya Burundi huku wakionesha mchezo safi uliokuwa ukiwainua mashabiki vitini kwenye uwanja wa Nyayo. Kocha wa Sudan Kusini amesema wanataka kuzifumba midomo timu moja baada ya nyingine, leo wanacheza na Tanzania na kesho Jumamosi itakuwa ni zamu ya Kenya hivyo lengo ni kuzimaliza timu zote hizo. Kwa upande wa Kenya jana ilitiwa hofu mwanzoni na Somalia kabla ya kuangushwa kwa102-77 katika michuano hiyo ambayo jana iliingia katika siku yake ya tatu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako