• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • China inaweza kudumisha hadhi yake ya kuongoza ukuaji wa uchumi duniani

  (GMT+08:00) 2020-01-17 18:23:52

  Idara Kuu ya Takwimu ya China leo imetangaza kuwa Pato la Taifa GDP la China limefikia dola za kimarekani trilioni 14.38, likiwa ni ongezeko la asilimia 6.1 kuliko mwaka jana wakati kama huo, na limepita lengo lililowekwa kati ya asilimia 6 na asilimia 6.5.

  Mafanikio hayo yamepatikana kwa kutegemea sifa ya China ya kuwa na soko kubwa. Kuwa na soko kubwa la matumizi lenye idadi ya watu bilioni 1.4, na kundi kubwa zaidi la watu wenye mapato ya katikati duniani, ni sifa ya kipekee ya China, na fedha hizo zinatosha kukidhi mahitaji ya ununuzi. Mwaka 2019, wastani wa mapato ya wakazi yanayoweza kutumiwa ulikuwa dola za kimarekani 4,480, kiasi ambacho kililingana na ongezeko la uchumi. Ni wazi kwamba matumaini ya wananchi wa China kwa maisha mazuri yamebadilishwa na kuwa msukumo mkubwa wa kuhimiza ongezeko la uchumi, hivyo kuboresha muundo wa uchumi na kuongeza uwezo wa China katika kukabiliana na hatari kutoka nje.

  Wakati huo huo sera mbalimbali za fedha za serikali, mageuzi ya viwanda vya taifa, na hatua za kuboresha mazingira ya biashara zilizotekelezwa katika miaka ya hivi karibuni zimeonesha ufanisi hatua kwa hatua. Mwaka 2019 ushuru uliopunguzwa kwa zaidi ya dola za kimarekani bilioni 280 nchini China, kiasi ambacho kimechukua zaidi ya asilimia 2 katika pato la taifa GDP, na kuongeza uhai wa viwanda. Pia katika kipindi hicho, viwanda vipya milioni 23.77 vimesajiliwa, na wastani wa idadi hiyo kwa kila siku imefikia elfu 20.

  Katika mwaka uliopita, China ilizidi kupanua ufunguaji mlango, na kuwa na uhusiano wa karibu zaidi na dunia, pia China iliongeza mara mbili kiwango cha kurudisha ushuru kwa baadhi ya bidhaa zinazouzwa nje ya nchi, na kupunguza ushuru kwa bidhaa za matumizi zinazoagizwa kutoka nje. China pia imeondoa ushuru kwa baadhi ya madawa yanayoagizwa kutoka nje, na kutilia maanani zaidi katika ufunguaji mlango wa kimuundo. Hatua hizo zimejenga imani ya wawekezaji wa kimataifa kwa uchumi wa China.

  Mwaka 2020, China itaendelea kushikilia kanuni ya kupata maendeleo yenye sifa bora, kudumisha ukuaji wa uchumi katika kiwango mwafaka, kuhakikisha mafanikio ya ujenzi wa pande zote wa jamii yenye maisha bora na utekelezaji wa mipango ya 13 ya miaka tano, na kuendelea kuwa injini yenye nguvu kubwa ya ukuaji wa uchumi duniani.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako