• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Mwakilishi maalumu wa China ahudhuria sherehe ya kuapishwa kwa rais wa Msumbiji

  (GMT+08:00) 2020-01-17 19:47:54

  Mwakilishi maalumu wa rais wa China ambaye pia ni naibu spika wa kamati ya kudumu ya bunge la umma la China, Bw. Cai Dafeng, Jumatano alihudhuria sherehe ya kuapishwa kwa rais Filipe Nyusi wa Msumbiji huko Maputo, na kukutana rais Nyusi Alhamisi.

  Bw. Cai alimkabidhi Rais Nyusi salamu za pongezi kutoka kwa rais Xi, na kusema China inapenda kushirikiana na Msumbiji kuimarisha uaminifu wa kisiasa, kupanua ushirikiano wenye ufanisi, kuhimiza uratibu kwenye mambo ya kimataifa na kusukuma mbele uhusiano wa wenzi wa ushirikiano wa kimkakati kati ya nchi zao.

  Rais Nyusi amesema Msumbiji inaishukuru China kwa kuunga mkono maendeleo ya uchumi na jamii kwa muda mrefu, na inapenda kuimarisha ushirikiano na China kwenye sekta za usalama, uchumi na biashara, na kuhimiza maendeleo ya nchi hizo mbili.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako