• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Shirika la ndege la Ehiopia lapanga kujenga uwanja mpya wa ndege utakaogharimu $5 bilioni

  (GMT+08:00) 2020-01-17 19:49:49
  Afisa Mkuu Mtendaji wa Shirika la ndege la Ethiopia ametangaza mipango ya kujenga uwanja wa ndege wa $5 bilioni kusini mwa Addis Ababa,Ethiopia.

  Tewolde Gebremariama alisema uwanja huo utajengwa katika eneo lenye ukubwa kilomita mraba 35 na utaweza kushughulikia abiria 100 milioni kwa mwaka.

  Shrika hilo la ndege linalomilikiwa na serikali,ambalo ndio shirika lenye faida kubwa barani Afrika,na ukubwa kwa kuwa na ndege nyingi,sasa hivi makao makuu yake ni katika uwanja wa Kimataifa wa Bole,uliopo mji mkuu wa Ethiopia,Addis Ababa.

  Ujenzi wa uwanja mpya wa ndege unatarajiwa kuanza baadae mwaka huu katika mji wa Bishoftu,ulioko kilomita 39 kusini mashariki mwa Addis Ababa.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako