• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Wakulima wa mahindi Kenya wataka kulipwa Sh4,000 kwa kila gunia la kilo 90

  (GMT+08:00) 2020-01-17 19:50:13
  Wakulima wa mahindi kutoka eneo la kaskazini mwa Bonde la Ufa,nchini Kenya ,sasa wanaitaka serikali kununua gunia moja la mahidni kwa Sh4,000 na ushei kutoka bei ya Sh2,500 ya mwaka uliopita.

  Hali hii imechangiwa na upungufu wa zao hilo unaotarajiwa kuyakumba maeneo mengi nchini Kenya baadaye mwakani..

  Wakulima pia wanaitaka serikali kupunguza masharti makali ambayo imewawekea wanapowasilisha mahindi yao kwa Halmashauri ya Kitaifa ya Ununuzi wa Nafaka (NCPB).

  Wamepinga vikali pendekezo la serikali kuwalipa baada ya kuwasilisha mazao yao kwa halmashauri hiyo.

  Wallisema wanaitaka serikali kununua mazao yao kwa bei nzuri,pengine Sh4,000 aua zaidi kwa gunia moja la kilo 90.

  Pia wametaka malipo yafanywe papo hapo wanapowasilisha mazao yao.

  Halmashauri hiyo inakumbwa na ushindani mkali kutoka kwa wasagaji, wanaonunua mahindi hayo kwa bei ya juu.

  Jana, wasimamizi wa maghala hayo walisema kwamba, watanunua mazao hayo kwa bei ya chini ya Sh3,200 ambayo ndiyo bei ya wastani wasagaji wananunua mahindi kwayo.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako