• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Tullow yafuta Sh3 trilioni katika uwekezaji wa Uganda, Kenya

  (GMT+08:00) 2020-01-17 19:51:09

  Kampuni ya kuchimba mafuta ya Tullow imefuta $800 milioni za gharama zake za utafutaji mafuta nchini Uganda na Kenya baada ya kushusha utabiri wake wa muda mrefu wa bei ya mafuta ghafi.

  Makampuni ya mafuta hurejesha gharama zao ndani ya miaka kadhaa baada ya uzalishaji na uuzaji wa bidhaa hiyo unapoanza ,huku bei za chini za mafuta zikiashiria kiwango cha chini cha kurejesha gharama za uwekezaji.

  Bei za mafuta ghafi zimekuwa chini ya $75 kwa pipa tangu mwezi Oktoba,2018,huku Tullow ikiangalia bei za sasa za bidhaa hiyo kama msingi wa bajeti yake.

  Kampuni hiyo imetumia zaidi ya $1 bilioni katika uchimbaji na utafutaji mafuta nchini Kenya pekee ,na haikubainika wazi ni kiasi gani kimefutwa.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako