• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Serikali ya Tanzania yaiomba China kuipatia ratiba ya maonyesho ya madini

  (GMT+08:00) 2020-01-17 19:51:30
  Serikali ya Tanzania imeuomba ubalozi wa China kuipatia ratiba za maonyesho ya madini nchini kwao ili wafanyabiashara wakubwa wa madini washiriki kwa ajili ya kutangaza aina za madini yalipyopo Tanzania.

  Ombi hilo lilitolewa jana na Naibu Waziri wa madini,Stanslaus Nyongo,wakati akifunga mkutano wa mabalozi wa China na Tanzania pamoja na wafanyabiashara wa madini ulioandaliwa na chama cha Wafanyabiashara wakubwa wa Madini (Tamida).

  Naibu Waziri Nyongo alisema wakipata ratiba za maonyesho hayo,itakuwa fursa nzuri kwa wafanyabiashara nchini Tanzania kutangaza madini yaliopo ambayo mengi hayajulikani japo ni mazuri nay a kipekee.

  Aidha aliwaambia wafanyabiashara watumie vizuri fursa hiyo kwa kutafuta soko la uhakika la madini ya Tanzania kwa sababu China kuna soko kubwa la madini.

  Pia aliagiza wafanyabiashara wakubwa wa madini walioko kwenye soko la madini la Arusha kuzipandisha hadhi ofisi zao ili kuvutia watalii wengi kuwatembelea na kununua madini hayo.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako