• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China na Myanmar zakubaliana kujenga jumuiya yenye hatma ya pamoja kati ya nchi hizo

    (GMT+08:00) 2020-01-18 18:03:38

    China na Myanmar zimekubaliana kutumia fursa ya maadhimisho ya miaka 70 tangu kuanzishwa kwa uhusiano wa kibalozi kati yao na kujenga jumuiya yenye hatma ya pamoja kati ya nchi hizo pamoja na kuhimiza uhusiano wao uingie kwenye zama mpya.

    Rais Xi Jinping wa China leo mjini Nay Pyi Taw amekutana na mshauri mkuu wa serikali ya Myanmar Bibi Aung San Suu Kyi. Kwenye mazungumzo yao, Bibi Aung San Suu Kyi amesema kiini cha uhusiano kati ya Myanmar na China ni kuheshimiana, kuelewana na kuungana mkono, na uungaji mkono unaotolewa na China kwa Myanmar haulengi kujipatia faida binafsi, bali ni kulinda usawa na haki. Amesisitiza kuwa kuna nchi zinazoingilia mambo ya ndani ya nchi nyingine kwa kutumia kisingizio cha haki za binadamu, kabila au suala la dini, lakini kamwe Myanmar haitakubali shinikizo na uingiliaji kama huo. Ametoa wito kwa China kuendelea kutetea haki za nchi ndogo na zenye ukubwa wa kati katika majukwaa ya kimataifa.

    Rais Xi Jinping amesisitiza kuwa China imekuwa ikishikilia kuheshimu wananchi wa nchi mbalimbali wachague wenyewe njia ya kujiendeleza inayoendana na hali halisi ya nchi zao, kushikilia kutoingilia kati mambo ya ndani ya nchi nyingine na kuunga mkono juhudi za Myanmar kulinda heshima na mamlaka halali ya nchi.

    Kwenye mazungumzo yao, rais Xi Jinping na Bibi Aung San Suu Kyi pia wamekubaliana kuimarisha ushirikiano kwenye ujenzi wa pamoja wa "Ukanda Mmoja, Njia Moja" ikiwemo maeneo maalum ya kiuchumi, barabara na reli pamoja na nishati ya umeme, na kusisitiza kuwa ujenzi wa ushoroba wa kiuchumi kati ya China na Myanmar ni kipaumbele kwenye "Ukanda Mmoja, Njia Moja".

    Rais Xi pia ametoa wito kwa China na Myanmar kupanua ushirikiano wa biashara na uwekezaji, na kusema China inaikaribisha Myanmar kuuza zaidi bidhaa zake nchini China, na pia itaunga mkono kampuni za China kuongeza kuwekeza nchini Myanmar.

    Wakati huohuo, nchi hizo mbili zimetoa taarifa ya pamoja zikisisitiza kuendelea kuongeza uratibu katika mashirika mbalimbali ya kimataifa ukiwemo Umoja wa Mataifa na kuungana mkono kwenye masuala yanayohusu maslahi makuu na ufuatiliaji mkubwa wa kila upande.

    Wakati huohuo, rais Xi pia amekutana na kamanda mkuu wa vikosi vya ulinzi vya Myanmar Min Aung Hlaing. Kwenye mazungumzo yao, rais Xi ametoa wito kwa majeshi ya nchi hizo mbili kushirikiana kujenga jumuiya yenye hatma ya pamoja kati ya China na Myanmar, na kufanya juhudi za pamoja kulinda amani na utulivu wa maeneo ya mpakani mwao. Na habari nyingine zinasema rais Xi Jinping wa China na viongozi wa Myanmar Ijumaa jioni walihudhuria hafla ya kitaifa ya maadhimisho ya miaka 70 tangu kuanzishwa kwa uhusiano wa kibalozi wa nchi hizo mbili na kuzindua Mwaka wa Utamaduni na Utalii kati ya China na Myanmar. Kwenye halfa hiyo, rais Xi amesema watu wa China na Myanmar wamefurahia uhusiano mzuri kwa maelfu ya miaka, akisisitiza urafiki mkubwa na utamaduni wa kukabili furaha na changamoto kwa pamoja.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako