• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Rais Xi ametoa wito wa uhusiano wa wenzi wa karibu kati ya China na Vietnam

  (GMT+08:00) 2020-01-18 18:04:01

  Rais Xi Jinping wa China amesema anapenda kufanya kazi na mwenzake wa Vietnam Nguyen Phu Trong ili kukuza kithabiti uhusiano wa pande mbili kwenye mwelekeo sahihi na kuinua uhusiano wa wenzi wa ushirikiano wa kimkakati wa pande zote katika zama mpya kwenye ngazi mpya

  Rais Xi ametoa kauli hiyo kwenye salamu zake za kupongeza miaka 70 ya kuanzishwa kwa uhusiano wa kibalozi kati ya China na Vietnam.

  Kwa upande wake, rais Nguyen Phu Trong amesema kwenye salamu zake za pongezi kuwa kuimarisha na kuendeleza vizuri uhusiano kati ya Vietnam na China ni wajibu wa kihistoria unaobebwa na pande mbili, na kunaendana na matarajio ya pamoja ya wananchi wa nchi hizo mbili. Amesema kuwa Vietnam siku zote inaweka kipaumbele uhusiano wake na China kwenye sera ya mambo ya nje, na imaamini kuwa uhusiano wa nchi hizo mbili unaimarishwa zaidi kutokana na uongozi wa viongozi wa vyama na wa nchi hizo mbili.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako