• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Afrika yatakiwa kurejea mafanikio ya AfCFTA katika mpango wa kunyamazisha bunduki

    (GMT+08:00) 2020-01-18 18:05:18

    Wakati viongozi wa Afrika wakitarajiwa kukutana mwezi ujao chini ya Umoja wa Afrika kujadili kuhusu kunyamazisha milio ya bunduki katika Afrika, wataalamu wametoa wito kwa watunga sera wa Afrika kurejea umoja uliopatikana katika makubaliano ya Eneo la Biashara Huria la Afrika AfCFTA ili kuondoa migogoro yote inayotishia matarajio ya maendeleo ya Afrika.

    Wito huo uliotolewa na Taasisi ya Mafunzo ya Usalama ISS, shirika lisiloingiza faida la Afrika, kwenye chapisho liitwalo "Migogoro bado ni changamoto kubwa ya Afrika katika mwaka 2020" umesisitiza umuhimu wa viongozi wa Afrika kurudia umoja uliopatikana kwenye biashara huria kunyamzisha milio ya bunduki.

    Kwa mujibu wa taasisi hiyo mwaka 2020 unapaswa kuwa mwaka wa alama kwa nchi wanachama 55 wa Umoja huo, wakati ambapo mpango mkuu wa Umoja wa Afrika barani humo, uitwao Kunyamazisha Bunduki unatetea "kumaliza vita vyote, migogoro ya wenyewe kwa wenyewe, ukatili wa kijinsia, mizozo na kuzuia mauaji ya kimbari katika bara hilo hadi kufikia 2020.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako