• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • ZTE ya China na MTN ya Uganda zaanza majaribio ya teknolojia ya 5G

    (GMT+08:00) 2020-01-18 18:05:39

    Kampuni ya teknolojia ya ZTE ya China na kampuni ya simu ya MTN ya Uganda zimeanza majaribio ya teknolojia ya 5G mjini Kampala na kuifanya Uganda itarajiwe kuwa nchi ya kwanza kutumia mtandao wa 5G katika Afrika mashariki.

    Katika hafla ya uzinduzi wa teknolojia hiyo, waziri mkuu wa Uganda Ruhakana Rugunda, aliyekuwa mgeni rasmi, amesema serikali inaunga mkono maendeleo ya teknolojia mpya iliyotolewa ambayo itatatua changamoto za watu na kufanya maisha kuwa rahisi na nafuu. Aidha ameeleza matarajio yake kwamba 5G italeta matokeo kwenye maendeleo ya uchumi nchini.

    Kwa upande wake mkurugenzi mtendaji wa Tume ya Mawasiliano ya Uganda Godfrey Mutabazi amesema wasimamizi wa sekta ya mawasiliano wanashughulikia kuhakikisha kwamba inakuwepo miundo mbinu itakayofaa 5G, na kuongeza kwamba Uganda itakuwa nchi ya kwanza Afrika Mashariki kuwa na teknolojia ya 5G na ya tatu katika Afrika baada ya Afrika Kusini na Nigeria.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako